Breaking News

MAJALIWA AZUNGUMZA KATIKA MARATHON YA KUMBUKUMBU KIFO CHA SOKOINE.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Napono Sokoine,  Mjane wa Waziri wa Mkuu  wa zamani, Marehemu, Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha  ambapo zilifanyika mbio za Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu  Edward Moringe Sokoine, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mtoto wa Marehemu Edward Sokoine, Mamelok Sokoine akitoa salamu za familia katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Edward Moringe Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019.
 
PMO 3745, PMO 3808, PMO 3819 na PMO 3821 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Sokoine   kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019.
 
Baadhi ya viongozi na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Marathon ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Wasanii wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipoozungumza katika Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha  Marehemu Sokoine kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. 

 
Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kuzungumza katika Marathon ya Kumbukumbi ya miaka 35 ya kifo cha Marehemu Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha Aprili 6, 2019.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. 
 
Majaliwa akimkabidhi Joseph Panga zawadi ya shilingi milioni moja ambaye aliibukuka kuwa Mshindi wa kwanza wa Marathoni ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya kifo cha Edward Moringe Sokoine, Kilomita 21 wanaume kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Aprili 6, 2019. Wa tatu kulia ni mshindi wa pili Alphonce Felix Simbu na Kulia ni mshindi wa tatuLazaro Damas. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa Shirikisho la Riadha nchini, Anthony Mtaka, Mjane wa Marehemu Edwad Moringe Sokoine, Napono Sokoine na wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments