MAABARA YA KISASA YA TAEC KUGHARIMU ZAIDI YA BILION 10.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki
Tanzania(TAEC) Profesa Lazaro Busagala akibadilishana mktaba wa muendelezo wa
ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa maabara ya TAEC, ujenzi wenye thamani ya
shilingi Bilioni 10,447,749,433.24
na Mkurugenzi wa Kampuni ya M/S LI JUN DEVELOPMENT COMPANY
LTD. maabara hiyo itajengwa kwenye makao makuu ya TAEC yaliyopo Njiro jijini Arusha
TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC)
September 10, 2019 imesaini mkataba wa shilingi bilioni 10,447,749,423.24 na kampuni
ya ujenzi ya M/S LI JUN DEVELOPMENT
CONSTRUCTION LTD kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili maabara ya kisasa.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu
za Atomiki Tanzania (TAEC) Profesa Lazaro Busagala ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha
inajenga maabara hiyo kwa kiwango cha hali ya juu kulingana na makubaliano ya mkataba
husika.
Maabara hiyo ni mwendelezo wa
maabara ya awamu ya kwanza iliyozinduliwa mwezi April mwaka huu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Ujenzi huu wa maabara ni juhudi zingine za serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika kuendelea kuleta maendeleo
nchini.
No comments