WATANZANIA WATAKIWA KUPINGA RUSHWA YA NGONO NCHINI
Baadhi ya watu waliojitokeza kwenye maadhimisho ya ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yenye lengo kujadili kampeni ya kutokomeza rushwa ya ngono nchini.
Na Mussa Khalid Dar es salaam
Watanzania
wametakiwa kuungana kwa pamoja katika kuvidhibiti vitendo vya ukatili wa
kijinsia wanaokumbana nao wanawake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya wahusika
wanapowabaini.
Wito huo
umetolewa leo Novemba 27,2019 jijini Dar es salaam na wadau kutoka taasisi
mbalimbali za wanawake katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa
kijinsia yenye lengo kujadili kampeni ya kutokomeza rushwa ya ngono nchini.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi wa wanawake Tanzania Marry
Rusimbi alisema kutokana na ukatili wa ngono kutoongelewa kila wakati
imepelekea waanzishe kampeni ya kukomesha vitendo hivyo.
Aidha
alisema wanakampeni ya muunganiko wa ushirika na wanaharakati mbalimbali uitwao
mtandao wa kupinga rushwa ya ngono Tanzania.
Awali akizungumza
Mwenyekiti kamati ya wanawake Shirikisho la vyama vya wafanyakazi
Tanzania Rehema Ludanga aliwata wafanyakazi wanaofanyiwa ukatili wa kingono
kujitokeza kutoa taarifa ili wasaidiwe kwa wakati.
“Baada ya
kuwa tumesema kwa muda watu wameanza kujtokeza hivyo naendelea kusisitiza
waendelee kujitokeza ili kutoa taarifa zitakazofanya kupata tawimu ya pamoja
“alisema Rehema
“Zamani
watu wengi walikuwa wanaona ni siri jambo hilo kwani mpaka sasa kwa takwimu za
nchi zinaonyesha ni asilimia 28 ya wanawake wananyanyasika kijinsia kwa mwaka
nasi wafanyakazi tunaingia katika gurudumu hili la nchi nzima”aliendelea
kusisitiza Rehema
Agnes
Lukanda kutoka Binti Leo Mtandao wa wasanii wanawake Tanzania alisema ni vyema
jamii ikaunga mfumo wa pamoja katika kupambana na vitendo vya rushwa ya ngono.
“Mini
ninacho kishauri ni kwamba tuangalie ni kwa vipi tunaweka mifumo ya wazi ya
utoaji huduma zilizobora itakayomfanya mwanamke asikamatwe na rushwa ya
ngono”alisema Lukanda
Maadhimisho
hayo yaliambatana na kauli mbiu isemayo “kataa rushwa ya ngono jenga
kizazi chenye usawa”yamehudhuriwa na maafisa wa TAKUKURU,Tanzania
Polisi,TAWAJA,WAJIKI ili kujadili ujenzi wa nguvu ya pamoja katika kuendeleza
vita dhidi ya Rushwa ya ngono.
No comments