Breaking News

RAIS MAGUFULI AMTEUA KAMISHNA DIWANI ATHUMAN MSUYA KUWA MKURUGENZI MKUU WA USALAMA WA TAIFA.

Rais Dkt. John Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba.


Ikulu, Dar es Salaam.

Raisw Dkt. John Magufuli amemteua na kumuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Uteuzi wa Kamishna Diwani Athuman Msuya umeanza leo tarehe 12 Septemba, 2019 na ameapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo,Kamishna Diwani Athuman Msuya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka Kamishna Diwani Athuman Msuya kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwakuweka mbele maslahi ya Taifa.

Kamishna Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine.

No comments