Breaking News

NEEMA ZANZIBAR, SMZ YAPATA GAWIO LA BILIONI 25



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 

Na Iddi Haji, Maelezo, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepatafaida  zaidi ya shilingi bilioni 25  ikiwa ni malipo ya  huduma za matumizi ya mkonga wataifa, SerikalimtandaoVisiwani Zanzibar

Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Mkonga wa Mawasiliano Zanzibar, Mhandisi Shukuru Awadhi Suleiman amesema kwamba fedha hizo zimelipwa kutoka katika makapuni ambayo yanatumia huduma zao.

“TumepatafedhahizoambazokutokaKampuniyasimuya ZANTEL ikiwanimalipokuanziamwaka 2013 hadimwaka 2024” AlisemaMkurugenzihuyo.

Alisema kwamba Serikali mtandao imekuwa nafaida kubwa kwa wananchi ambapo sasa huduma zaa fya, kodi na elimu zimekuwa zikitolewa kwa urahisi na ufanisi mkubwa.

Amesema katika sekta ya afya, kumekuwa na mafanikio makubwa katika huduma, vituo vya afya 24 Unguja na Pemba vimeunganishwa katika mfumo wa Serikali mtandao.

“Leo hii mgonjwa anaweza kufanyiwa vipimo kama vya X-ray katika hospitali ya Kivunge Mkoa Kaskazini Unguja  na, vipimo vile vitasomwa Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja bila ya mgonjwa au daktari kulazimika kusafiri” Alisema Mkurugenzi Mhandisi Shukuru.

Mkurugenzi huyo amesema kwa kutumia huduma za Serikali Mtandao, huduma za vyeti vya kuzaliwa imekuwa rahisi kwa sasa kwani wananchi wanapata vyeti vya kuzaliwa katikaWilaya zao.

“Sasa hivi Wakala wa Usajili na Matukio ya Kijamii Zanzibar  wanatumia huduma hizi, watu wanapata vyeti vyao vya kuzaliwa katika Wilaya zao, wanaomba huko na taarifa zao zinatumwa Makao Makuu na kufanyiwakazi” Alisema Mkurugenzi Shukuru.

Mbali ya sekta hizo, pia Kampuni ya Uunganganishaji Maudhui ya  ZMUX inatumia mkonga wataifa katika kurusha matangazo ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Akizungumziasektayakodi,Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kwamba Bodi ya Mapato Zanzibar nimoja yawatumiaji wakubwa wahuduma za Serikali mtandao ambapo sasa huduma za kodi zimeunganishwa katika mtandao mmoja.
Mwisho.

No comments