Breaking News

RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA DODOMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Dodoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma katika eneo la Nzuguni leo tarehe 22/11/2019 jijini Dodoma. Miradi mingine ambayo Rais Mgaufuli ameweka jiwe la Msingi ni mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Uhuru Chamwino, Ujenzi wa Soko la Kisasa , Nyumba za Askari Polisi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mke wake, Mama Janeth Magufuli  mbele ya wananchi wa Dodoma alipokuwa na akizungumza na wakazi wa Dodoma mara baada  ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma katika eneo la Nzuguni leo tarehe 22/11/2019 jijini Dodoma





Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019.


 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge akielezea nyaraka ambazo wamekusanya kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya ardhi wakati wa hafla ya Uwekaji jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo tarehe 22/11/2019. Nyaraka hizo alimkabidhi Mhe. Rais Magufuli ili iwe rejea atakapo kutana nakatika jiji la Dodoma.  changamoto na malalamiko kuhusiana na migogoro ya ardhi 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma katika eneo la Nzuguni leo tarehe 22/11/2019 jijini Dodoma

No comments