TANTRADE YASAIDIA KAMPUNI 31,891 KUPATA TAARIFA ZA BEI YA MASOKO NA BIDHAA
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade), Bi. Latiffa Mohammed, akizungumza na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani), kuhusu Mafanikio ya TANTRADE kwa maiaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
DAR ES SALAAM
27.11.2019
MAMLAKA ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) katika kipindi cha miaka minne ya
Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuziunganisha kampuni 31,891
kuweza kupata taarifa za bei na masoko ya bidhaa za ndani na nje ya
nchi.
Hayo yamebainishwa
leo Jumatano (Novemba 27, 2019) Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkurugenzi Mkuu
wa TANTRADE, Latifa Khamis wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya
Taasisi hiyo katika Kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya
Tano kuanzia Novemba 2015 hadi Novemba 2019.
Alisema kuwa ya
wafanyabiashara hao, TANTRADE iliweza kuunganisha katika masoko
wafanyabiashara 405 na kuuza tani 102,000 za mahindi, tani 2,000 za
karanga, tani 5,000 za soya, tani 50 za ufuta, tani 7 za majani ya papai,
kilogramu 200 za unga wa ubuyu, tani 2 za iliki, tani 5,000 za muhogo na tani
3.2 za tangawizi ya unga.
Aliongeza kuwa
miongoni mwa bidhaa zilizoonesha uhitaji mkubwa katika masoko ya nje ni pamoja
na matunda, samaki na mazao ya bahari, jamii ya mikunde, asali, kahawa, chai,
korosho, viungo na vyakula, ambapo maulizo ya bidhaa hizo yalitoka katika nchi
za India, Nchi za Kiarabu, Misri, Marekani, Vietnam na Ulaya.
‘’Mbali na
kusambaza taarifa za uhitaji wa bidhaa mbalimbali TANTRADE kwa kushirikiana na
wanunuzi kutoka nchi zao tumewezesha kupatikana kwa muendelezo wa kimkakati wa
kupenya katika masoko yao, semina mbalimbali ziliratibiwa ambapo
wafanyabiashara na wadau 425 walishiriki ili kutambua fursa za masoko ya nje na
taratibu za kuyafikia’’ alisema Latifa.
Kuhusu ukuzaji
na uendelezaji wa masoko ya nje ya nchi, Latifa alisema TANTRADE imeendelea
kuratibu maonesho ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) kwa lengo la
kutoa fursa za kutangaza bidhaa zilizoongezewa thamani na upatikanaji wa
teknolojia ili kupanua wigo wa masoko ya nje ya nchi.
Latifa alisema
kupitia DITF kila mwaka Tanzania hupokea wastani wa kampuni
500 kutoka zaidi ya nchi 35 zinazoshiriki maonesho hayo na hivyo
kuwasaidia wafanyabiashara katika upatikanaji wa teknolojia na kusaidia kutatua
changamoto za uzalishaji hafifu wa bidhaa za kilimo, uchenjuaji wa madini na
hivyo kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa.
Akifafanua zaidi
Latifa alisema kwa mwaka 2019 pekee kupitia DITF, mafanikio mbalimbali yaliweza
kupatikana ikiwemo kampuni 437 kupata oda ya kufanya biashara zenye thamani ya
Tsh Bilioni 7.93, kufanyika kwa mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya wastani
wa Tsh. Milioni 209, pamoja na kutengeneza ajira za muda mfupi zipatazo 14,912
zilizotokana na kazi mbalimbali za maonesho ikiwemo ujenzi, ulinzi na usafi.
Akizungumzia
kuhusu ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya nje ya nchi, Latifa alisema
Tanzania imefanikiwa kushiriki katika maonesho katika nchi zilizo na utengamano
ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo wastani wa kampuni 200 zimeweza kushiriki na
kutambua bidhaa zao kwenye nchi hizo na kuingia mikataba ya kibiashara ili
kupata masoko endelevu.
Akitoa mfano
Latifa alisema katika mwaka 2018/19, Tanzania ilishiriki maonesho ya 15 ya
Biashara China ambapo kampuni 20 zilishiriki na kuweza kutafutiwa masoko ya
bidhaa na kutangaza vivutio mbalimbali vya uwekezaji ikiwemo vivutio vya
utalii, mazao ya kilimo hususani kahawa, chai, karafuu, asali, korosho, mazao
ya jamii ya kunde na bidhaa za mikono ikiwemo vikoi.
‘’Katika
maonesho ya chakula ya Gulfood-Dubai kampuni tatu zaTanzania zilifanikiwa
kutembelea maonesho hayo yaliyofanyika Dubai kwa lengo la kutambua fursa
mbalimbali kutoka kwa washiriki, ambapo wanunuzi wa bidhaa mbalimbali kama
asali kontena 30, kahawa tani 50, ukwaju tani 10 walipatikana’’ alisema Latifa.
Aidha Latifa
alisema TANTRADE katika kutekeleza adhima ya Tanzania ya Viwanda ilianzisha
maonesho ya bidhaa za Viwanda vya Tanzania yanayofanyika kila mwezi Desemba,
ambapo tangu kuanza kwake mwaka 2007 wastani wa makampuni 497 hushiriki na
kuwafanya wazalishaji wa bidhaa nchini kupata fursa ya kutambulisha bidhaa zao
na kuhamasisha matumizi ya bidhaa za Tanzania.
MWISHO
No comments